Released on November 13, 2014

35K Views

Thumbnail

Intro:

Hahahhaa

13

Bongo Records..


[Verse 1: Msodoki]

Mama ndiye alinitabiri mi nitakuwa staa na nyota kila pande

Nikiwa na raha, kama nina hasira nisijigambe

Usimpige mkeo, piga shangwe!

Maana Young Killa sio ngazi, kwa hiyo mwambieni shetani asinipande

I think big, is my dream big kuwa bigga wa michano

Ni**a ambae tajiri atanijua kuwa msodoki nawaficha mistari

Upeo wangu umekula mchicha na ndiyo maana nna fikra za kuona mbali

Msukuma naye sukuma mitikasi inatulia

Hata Francis Cheka naweza mpiga punch akalia

Wanayoijua njaa ndiyo wanaamini cha kwanza kilimo

Mi sitaki gombania u-star ili nikifa nikazikwe kino

Wabovu wakichana, imoo, na hawajui nguzo tano

Leo kwenye u-star simo kisa sina muonekano

Mi nna-power, ya ibada niliyo iomba baada ya kuipata

Pole dada ulienitosa kisa umenizidi kidato

Futa jasho na damu, saka noti, hali tete

Watoto wanamjua Diamond na joti zaidi ya Kikwete

Popote niko fiti, tega sikio

Shoga hata akitoa jicho vipi, hawezi akayaona mafanikio ndiyoo


[Hook: Belle 9, Fid Q & Msodoki]

Msodoki na Ngoshaa

Ndiyo miujiza iliyotabiriwa

Haina haja ya kuogopa

Nafasi nilizozichezea yawezekana zisirudi

Lakini naweza zitengeneza nikiongeza juhudi

Tangu Agosti, Tangu Aprili, 13

Tangu Agosti, Tangu Aprili, 13

Na-hustle bila wasi wala hofu

Ubongo hauwezi nipa shida ambayo ntashindwa kuisolve


[Verse 2: Fid Q]

Wakishaamini unawahitaji zaidi ya wanavyo kuhitaji

Mapenzi ya wadau wa mjini hugeuka samaki na maji

Kuishi ndani yake tu, nje yake uvuliwe

Kwa msaada wake upigwe, kisha anawishe uliwe

Sikuumbwa nije ku-settle for less

Naisubiri mvua inyeshe nijitokeze ku-dance

Non sense sitemi, asset siyo deni

Homeboy, natema vitu on point, jifunzeni

Thamini huu muda kabla hujageuka history

Part of the past don't fit the script for the future memory

Niliyo ya pitia yameniandaa kwa haya yajao

Siyo dalili ya kusinzia, ni njaa nikipiga mihayo

Sina jeuri wala mzaha kugeza tabia mbovu

Nna kiburi cha jeraha ukinipoteza naacha kovu

Maskini najiamini hadi natokwa na ukungu

Bila ujuzi wasinge ni thamini ningetoswa mpaka na ndugu

Kitacho nizamisha siyo kudondoka mtoni

Ni kushindwa kupiga mbizi, nakusizi ili msinione


[Hook: Belle 9, Fid Q & Msodoki]

Msodoki na Ngoshaa

Ndiyo miujiza iliyotabiriwa

Haina haja ya kuogopa

Nafasi nilizozichezea yawezekana zisirudi

Lakini naweza zitengeneza nikiongeza juhudi

Tangu Agosti, Tangu Aprili, 13

Tangu Agosti, Tangu Aprili, 13

Na-hustle bila wasi wala hofu

Ubongo hauwezi nipa shida ambayo ntashindwa kuisolve


[Verse 3: Fid Q & Msodoki]

Fid Q:

Napenda umaarufu, nachukia mbwembwe zake

Unapospit truth kwa boothe afu wa-kush hamninyaki

Nawaacha uchi, ukweli uzushi siyo mwake

Hata mkighushi mtafeli hamnigusi na hamnipati

Msodoki:

Siamini nimekuwa mimi hadi leo nimefika hapa

Alionilea hakuniamini, niliyemtegemea hakunitaka

Bila nyinyi, wadau nakiri sishiki sarafu

Na ndiyo maana sili bata, kwa maana bata wachafu

Kuwa mkali wa kusifiwa, kubali kutumiwa

Nilichoambiwa kuwa siku hizi hadi wajanja wanaliwa

Inatakiwa kuwa streka, mambo yaende shkopa

Kama hujanileta huwezi nirudisha nilipotoka

Outro:

Kumi na Tatu

Kumi na Tatu

Msodoki na Ngoshaa

Tangu Agosti, Tangu Aprili, 13

Tangu Agosti, Tangu Aprili, 13