TARGET

By SLIMSAL

Released on August 19, 2019

Thumbnail

Intro

Watakwambia anga ni kikomo angalia juu … eh

Waulize mbona mwezini kuna alama za miguu … whoa!

Wao wanakutaka wewe kwao ndio target … yea mh!

Nachotaka mimi nikuoneshe wewe target… Woo!

Verse 1

Waafrika wanawatolea macho waamerika

Waamerika wanawatoa macho waafrika

Wenye nacho na wasonacho sayansi ya matabaka

Waulize wenye nacho ni wapi walikipata

UsiulIze waso nacho ni wangapi wanakitaka

Sema kipo wapi uone ni wangapi watakifata

Upo sokoni kama msomi wa chuo kikuu

Kwenda kujiuza kwenye interview

Na hii picha View, ka ni picture of you

Jua una fikra Few mwambie Boss FU

Haijalishi hata kama hujawahi kwenda school

Ama ulikwenda na ukaambulia FF tu

Wakikwambia njoo tukemee madawa ya kulevya

Waambie tumtafute yule anayeyatengeneza

Huwenda tukaweza kuelewana kingereza

Kwa maana si hatumjui nani anayeyapenyeza

Chorus

Watakwambia Anga ni Kikomo Angalia juu yeaa… (Juu Juu Juu Juu yeaa)

Waulize mbona mwezini kuna alama za miguu yeaa… (Guu Guu Guu Guu yeaa)

Wao wanakutaka wewe kwao ndio target‚ Nnachotaka mimi nikuoneshe wewe target

Wao wanakutaka wewe kwao ndio target‚ Nnachotaka mimi nikuoneshe wewe target

Verse 2

Wakionesha alama peace‚ hakuna aliye salama

Sababu ni alama ya pistol, vidole vikikutana… yea!

Kule ulipokimbia ndipo ukweli ulipofichwa mh!

Maisha ya mtaani ni degree kibao ulimwengu ticha mh!

Mlango wa sita wa fahamu ndio ufunguo wa maisha

Zero mpya zipo Instagram facebook twitter

Mtandao ndo mtindio wa ubongo usiojificha

Mtandao ndio mtandio wa uongo unaouficha

Na Siku moja, nitarudi Kule tulipotoka

Nikawaeleze washkaji zangu kuwa tulipotoka

Na ndoto za kujenga maghorofa kwenye vichwa vya watoto wa kota yea!

Ndoto za kuwa mwanamuziki nyota bongo movie na kucheza soka Je?

Wapi zile ndoto za kusoma kuja kuwa lawyer ama kuwa doctor… Whoa!

Uuh! Shule haikunipa nilichokosa‚ Mitihani haikunipima ilini-torture

Walimu walinifunza kuwa mwoga, kwasababu niliwaogopa

Chorus

Watakwambia Anga ni Kikomo Angalia juu yeaa… (Juu Juu Juu Juu yeaa)

Waulize mbona mwezini kuna alama za miguu yeaa… (Guu Guu Guu Guu yeaa)

Wao wanakutaka wewe kwao ndio target, Nnachotaka mimi nikuoneshe wewe target

Wao wanakutaka wewe kwao ndio target‚ Nnachotaka mimi nikuoneshe wewe target