MUDA

By SLIMSAL

Released on January 15, 2018

Thumbnail

Sikuwa na ndoto kuishi Maisha ya mtaani kwenye kona

Japo siwadharau washakaji wa mtaani kwenye kona

Wala sijasahau kutoa tano nikiwaona

Kuwatoa tano tano washkaji zangu sioni noma

Najua imekuwa kitambo flani washkaji hawajanisoma

Wanauliza nimemuachia nani flag la Dodoma

Wakiuliza nimemuachia nani flag la Dodoma

Nawauliza mlipatia nani flag la Dodoma

Najua imekuwa muda Sina tena muda wa kupoteza muda

Kama nilioupoteza muda nilipokuwa mbele ya muda

Muda nilopoteza ndo umenifunza kutunza muda

Sina tena muda wa kupoteza muda huu ndo muda

Nilipokuwa darasani sikufundishwa kuhusu hela

Nilipoingia mtaani nilihisi kama nipo ndani ya jela

Nilipopata hela nilitaji tena hela

Nilipohitaji hela tena sikuipata tena hela

Baba kanifunza kujitegemea bila msaada

Mama akanifunza kumtegemea mungu baba

Pia Ulimwengu ndio mama ulionilea kama baba

Hii Dunia ina siku moja we unahesabu siku saba

Japo jana nilikosea njia, lakini leo sina tena hofu ya kupotea

Nauthamini muda mchache uliobakia

Sababu nyuma kuna muda mwingi uliopotea

Sigeuki tena nyuma kuangalia

Sababu mbele kuna mengi yanayoningojea

Na Huu sio muda kunivulia sidiria kisa pene

Huu sio muda wa kuchezea mpira na hawa vicheche

Huu sio muda wa kumsujudia pusha mwenye kete

Huu sio muda wa kusubiri hadi kidole kiwe na pete

Huu sio muda kumlilia shida Jakaya Kikwete

Huu sio muda wa kusubiri huyu aliyefika asepe

Huu sio muda wa kutumia akiba aliyokwambia uiweke

Ambayo uliitumia kabla ya shida na hali tete

Sikuwa na kitu kwa sababu sikuwa na kitu cha kufanya

Sikuwa na kitu cha kufanya sababu sikuwa na kitu, HAPANA

Uvivu ni kulala usiku ili kuusubiri mchana

Tusipende kutafuta majibu kwa kuulizana

Maisha yangu sio kuandika verse na kutoa wimbo

Maisha yangu ni kutoka pale nilipokuwa nipo

Na kutoka pale nilipokuwepo mpaka hapa nilipo

Sio safari ya karatasi kwenda na upepo mzito