Released on November 25, 2022

Thumbnail

[Verse 1 : Fari By Dar Kid]

Kama itatokea siku, utanimiss mie

Namba yangu ile ile naomba unipigie

Kama umepata muda unitembelee

Si kwa ubaya ila, hali tu unijulie

Vita vya ukimya tuliopigana mimi na wewe

Nimekiri nimeshindwa mimi bado ni yule yule

Uliugusa moyo wangu nakuleta tofauti pale

Kwenye kapu langu la hisia nafasi nyingine unipatie

Ooh, hakuna wakulijaza pengo lakooo

Moyo mtima unatamani pendo lako

Nipendwapo napajua ndio maana napajali

Maumivu yako nayatambua nimechoka kuwa mbali

Na kumiss kumiss honey wewe

Sio rahisi rahisi kuwa mwenyewe


[Chorus : Fari By Dar Kid]

Nipigie nipigie

Nipigie nipigie

Nipigie hata kidogo nikusalimie

Nipigie nipigie

Nipigie nipigie

Nipigie japo hali nikujuliе


[Verse 2 : Rayvanny]

Kama ukipata muda

Sauti yangu uisikie

Msimamo wangu ule ule

Kisa au sеma nirudie

Kama ukipata wasaa usinizungumzie

Si ulipata wengine mie niache usinifikirie

Sura yako maridhawa umeizalilisha

Kwa tabia yako

Niache niache baki peke yako

Moyo wangu umeugawa umenihuzunisha

Basi fanya yako

Niache niache mwana wa mwenzako

Kwani nilikupenda kwa dhati

Nikaapa sikuachi mtoto ulo smart

Penzi lis'o na bahati limefika tamati

Sa' nahesabu mabati

Maadui kindakindaki umewapa nafasi

Sa' wananidhihaki

Upendo umekaangwa chapati

Ushaunguza basi kuwa nawe sitaki

Niaaacheee


[Chorus : Fari By Dar Kid]

Nipigie nipigie

Nipigie nipigie

Nipigie hata kidogo nikusalimie

Nipigie nipigie

Nipigie nipigie

Nipigie japo hali nikujulie