PROFJ

Una suranzuri

Na tabia ya Kuvutia

Unaweza ukaishi popote katika hii dunia

Una tabasam pana la huba, sauti nyororo

Kweli kwako na kiri umenifunga minyororo

Siwezi kuita hii ni limbwata hata

Mi nabisha kwenye hili swala mi nakataa

Una sura ya mviringo

Mzuri huna maringo

Wallet imenenepa mithili ya mama bingo

Una - Meno yaliyo banana huna pengo wala mwanya

Kidani cha ulimi mama nacho hunichanganya sana

Una Macho macho madogo yasiyo hitaji miwani

Hani kiukweli kweli umeni kamata jamani

Una -Shingo ya kuvaa cheni nyembamba kiasi kwamba

Unatishia sana namba kwa wote wanaojigamba

Una Macho legevu utadhani umevuta wida

Ni kama baba lita walamoja demivida

Una chuchu kiduchu daima zanipa uchu

Simezi simung’unyi nahema tu nusunusu

Una hips kama umeficha panya ,unanichanganya

Daima we ni wangu wa kufa na kuzikana

Kiitikio

Una-Ngozi laini tema ya kung’aa

Una- Niua zaidi na hilo bambataa

Una-sifa zote ambazo mi nazipenda

Napenda tuwe wote kila seheme unayo kwendax2

Ngwair

Eyo nazizi, masham sham kwako simalizi

Nabalizi, unangozi kama ya Naziz

Macho ya kijapanizi

Kwako nishafika nafsi yangu imekita

Kifuani chuchu saa sita, machoni mtoto unaniita

Binti umejaliwa busara uzuri na utashi

Una nakshi napenda harufu yako nzuri ya marashi

Malkia wa moyo wewe pekee ndio fahari ya nafsi

Usiuwe na wasi, njoo sogea karibu yangu basi

Najiona niko ndotoni, nadeka kama utotoni

Mwingine kamwe sioni nakupenda toka moyoni

Una jicho la kleopatra mtoto hujui kunata

Mwanya kama aminata ndomama mwenzio nadata

Una tumbo dogo lenye mvuto sio kitambi

Unajua kubembeleza kwa lugha isiyo na komandi

Una midomo kasuku na joto lenye hisia

Dia una rangi yenye mng’aro na nuru isiyo fifia

Sikia, ujenzi wa mapenzi unakwenda ngazi kwa ngazi

Niamini nikuamini ili tuyaepuke maradhi

Kiitikio

Una-Ngozi laini tema ya kung’aa

Una- Niua zaidi na hilo bambataa

Una-sifa zote ambazo mi nazipenda

Napenda tuwe wote kila seheme unayo kwendax2

PROF J………

Una akili zaidi ya Linkoni, na unapenda kusoma

Kwanza unatafakari kwa yote unayo yaona

Hutazami tu ya leo unafikiri na Kesho

Hata usipoelewa unaomba kueleweshwe

Kitovu cha Kuweka pini mguu wa kimini

Umekaa sanaa akilini niamini fukara mimi

Miguu mithili ya chupa ya bia aina ya taska

Heshima na mapenzi ya kweli yasiyo na mafuta

Ngozi laini udhani naskrachi vocha

Midomo yako na ulimi huwo ni uchawi tosha

Una nibamba sana kwa jinsi ulivyo stable

Una thamani zaidi ya mpira mweusi wa pull table

Mikono yako laini ya kushika simu ndogo

Nahisi, utumbo wako haupitisi mihogo

Hakika wewe ni wangu tuzo maishani mwangu

Daima unastahili kuwepo ubavuni mwangu

Kiitikio

Una-Ngozi laini tema ya kung’aa

Una- Niua zaidi na hilo bambataa

Una-sifa zote ambazo mi nazipenda

Napenda tuwe wote kila seheme unayo kwenda x2