Nikusaidiaje

By Prof. Jay

Released on January 1, 2005

7K Views

Thumbnail

[Verse 1]

Umesahau ulipotoka, hujui unapokwenda

Ukapata kiburi kuona mi nakupenda

Nilikuthamini na letu penzi kulienzi

Na leo siamini kama umenisaliti mpenzi

Kumbuka nilikukuta kijijini Sitimbi

Umebeba mahindi na furushi la magimbi

Nguvu ziliniishia mithili ya kufa maji

Nafsi nayo ikakidi kwamba mimi nakuhitaji

Kigoli mwenye umbo kama la mdori

Wala sikutaraji ungepiga nami story

Nilifurahi kuweza kukufahamu

Na nikakuahidi subiri zangu salamu

Kwa kuwa nilikwenda tu kumtembelea bibi

Yote yaliyojiri tu kumweleza ilibidi

Wote walishangaa kusikia nataka mchumba

Kwani vijana wengi wa mjini tuna kasumba

Wakaweka kikao ndiposa niweze kutoa posa

Niliapa kujiua iwapo ningekukosa

Walinikabidhi nirudi nawe mjini

Na nikakusisitiza mjini kuwa makini


[Hook]

Nafsi yangu nilikupa uitunze mpenzi

Anasa za jiji zikakuchanganya

Mapenzi ukasaliti na ukanikana

Ukaniacha dunia ikiniandama

Kuwa nawe haitawezekana mpenzi

Nshampata ambae tunapendana

Majeraha makubwa yajadui moyoni

Mi nimeshamuachia Maulana


[Verse 2]

Alikuwa mzuri mithiri ya malaika

Alipotua mjini Zubeda ni patashika

Hakika alionekana alikuwa mgeni wa jiji

NIlipovua viatu nilivikuta ndani ya friji

Alifanya vibwenga washikaji wakanicheka

Hakutaka kitanda alilala kwenye mkeka

Alipokuwa akiona magari alikimbia

Akimuona mtu kwenye TV anamwamkia

Kila alichofanya alikuwa anakosea

Nilimvumilia kwa kuwa hajazoea

Hakai kwenye sofa, alikuwa anakaa chini

Mafuta ya kupikia eti anayapaka mwilini

Namnunulia soda hataki, anataka togwa

Nikimletea keki hataki, anataka boga

Majirani walimpenda sababu ya uzuri wake

Nasikitika mashangingi wakawa rafiki zake

Akaanza kunywa pombe alipokwenda kusuka

Usiku ananitoroka tena kwa kuruka ukuta

Nilipokuwa natoka, nae nyuma antoka

Nikimtuma kitu anadai eti amechoka

Nikienda kazini ndani analeta mabwana

Magari ya kifahari yakawa yanapishana

Hakika starehe za dunia zikamtenda

Na hatimaye hata nyumbani pia akatoweka


[Hook]

Nafsi yangu nilikupa uitunze mpenzi

Anasa za jiji zikakuchanganya

Mapenzi ukasaliti na ukanikana

Ukaniacha dunia ikiniandama

Kuwa nawe haitawezekana mpenzi

Nshampata ambae tunapendana

Majeraha makubwa yajadui moyoni

Mi nimeshamuachia Maulana


[Verse 3]

Nilipigwa na butwaa, mtaani walinishangaa

Nilikosa raha hata nafsi ilikata tamaa

Sikujua huyu binti ni mzima au amekufa

Ilibidi niombe watu msaada wa kumtafuta

Kumbe anaonekana viwanja vya kila aina

Leo yuko na mzungu na kesho yupo na Mchina

Nilipata shahuku ya kutaka japo kumuona

Ingiwa niliamini moyoni ingenichoma

Kweli tulimtafuta kwenye kumbi tofauti

Ili nihakikishe kweli hajapatwa na mauti

Nikamkuta casino la Wadachi na Walatino

Akigonga mvinyo, wa hashipapi, hashipinyo

Pechiechipinyo na pamba za mandarino

Macho yalinitoka mithiri ya zingonginyo

Hakika alipendeza kwa staili alizocheza

Na kila aliyemtazama alitamani kumchombeza

Kwa pozi na dharau alijifanya amenisahau

Akaniona takataka mbele ya washikadau

Ilibidi niondoke machozi yakinilenga

Shetani kashanitega na tunda langu kamega

Akapata mimba aliyempa hakumtambua

Na wote aliowafata eti wakakana kumjua

Zubeda na mimba yake hakuwa na pakuishi

Hakujua ale nini na vipi apate ridhiki

Ghafla hifadhi yake ikawa ni stendi ya basi

Siku nyingine mvua ilimnyeshea kupita kiasi

Akarudi nyumbani eti arudiane nami

Kurudi kwao hataki, mi na familia ndani


[Hook]

Nafsi yangu nilikupa uitunze mpenzi

Anasa za jiji zikakuchanganya

Mapenzi ukasaliti na ukanikana

Ukaniacha dunia ikiniandama

Kuwa nawe haitawezekana mpenzi

Nshampata ambae tunapendana

Majeraha makubwa yajadui moyoni

Mi nimeshamuachia Maulana