Niamini

By Prof. Jay

Thumbnail

Niamini (Sema)

Nataka uwe na mimi (Mama)

Watu wenye fitina wanaleta majungu uachane na mimi (Ye, ye, ye)

Hivi kwanini (Sema)

Hutaki kuniamini (Mama)

Nyoyo ziko pamoja mpaka siku ya kifo uanze we au mimi (Ye, ye, ye)

Niamini (Sema)

Nataka uwe na mimi (Mama)

Watu wenye fitina wanaleta majungu uachane na mimi (Ye, ye, ye)

Hivi kwanini (Sema)

Hutaki kuniamini (Mama)

Nyoyo ziko pamoja mpaka siku ya kifo uanze we au mimi (Ye, ye, ye)

Nakupenda sana ingiwa wanakuita demu wa uswazini

Penzi lako la kweli ndo kitu nachothamini

Kipepeo cha moyo we sema unachotaka

Jinsi unavyoenzi kipenzi sina mashaka

Tulipanda milima tukaja kwenye mabondе

Na sasa ni tambarare tufanye wanga wakonde

Kotе tunakopita wamemwagia mbigiri

Njoo nikumbatie tufe tukiwa wawili

Hushangai, tukigombana tu wanafurahi

Na tukiwa pamoja wanashindwa kutusabahi

Walishakuja kwangu kunipa habari zako

Nikawatoa mbio kulinda heshima yako

Kwangu wamenishindwa wamegeuza kibao

Changanua mapema upime akili zao

Ni maisha yo Liz, twende tujikongoje

Maisha safari ndefu sijui mbele kukoje

Wanasema mi nakunywa wee, nalala kwenye baa

Wanasema mi ni bingwa la ngono kwenye mitaa

Wanasema mi nimeshawataka wamekataa

Kwako napiga goti yoh twende ki-superstar

Niamini (Sema)

Nataka uwe na mimi (Mama)

Watu wenye fitina wanaleta majungu uachane na mimi (Ye, ye, ye)

Hivi kwanini (Sema)

Hutaki kuniamini (Mama)

Nyoyo ziko pamoja mpaka siku ya kifo uanze we au mimi (Ye, ye, ye)

Niamini (Sema)

Nataka uwe na mimi (Mama)

Watu wenye fitina wanaleta majungu uachane na mimi (Ye, ye, ye)

Hivi kwanini (Sema)

Hutaki kuniamini (Mama)

Nyoyo ziko pamoja mpaka siku ya kifo uanze we au mimi (Ye, ye, ye)

Yoh, nikwamba

Mi nashukuru sana, umeniamini kwa sana

Hukufata maneno ya wanga waliochonga kwa sana

Miss Manana baab kubwa, hiyo ndo dhana

Wala hukunikana asante sana mi sitokukana

Tulifarakana tulikaa chini, tukapatana

Bila kugombana na ndio maana hatujatengana

Tukasamehana bila kutosana, endelea kukazana

Visa vizabina maji ya shingo sa chupi zinabana

Vichwa vinagongana wanaulizana, hatujaachana

Wanapigwa na bumbuwazi kuona bado tunakumbatiana

Tunashirikiana, na tunafanya vitu vya maana

Na haki ya Mungu nakuahidi mi ndo wa dhamana

Nakata mzizi wa fitina we ni wangu wa kuzikana

Mwingine hakuna, vita vya manyoya sasa hapana

Kwani maneno yalizidi hasa kwa wanga na mahasidi

Na wengine waliahidi lazma watumwagie acid

Eti hakomi kutupwa na napiga sana mchupa

Hautachukua round kwangu mi ntakutupa

Haukufanya pupa haukuogopa, hungenichoza

Ya Mungu mengi leo hii kwetu mambo ni super

Na yote aliyoahidi kwako mimi lazima nitakupa

Usiwe na pupa, tulia, mi ndo simba

Unanipaga hamu, na hilo napenda ufahamu

Nakumbuka maneno yako matamu, mi nakupenda wewe

Unanipa kiwewe, ubavu wangu wa pili ni wewe

Napenda uelewe, niamini ni mimi na wewe

Niamini (Sema)

Nataka uwe na mimi (Mama)

Watu wenye fitina wanaleta majungu uachane na mimi (Ye, ye, ye)

Hivi kwanini (Sema)

Hutaki kuniamini (Mama)

Nyoyo ziko pamoja mpaka siku ya kifo uanze we au mimi (Ye, ye, ye)

Niamini (Sema)

Nataka uwe na mimi (Mama)

Watu wenye fitina wanaleta majungu uachane na mimi (Ye, ye, ye)

Hivi kwanini (Sema)

Hutaki kuniamini (Mama)

Nyoyo ziko pamoja mpaka siku ya kifo uanze we au mimi (Ye, ye, ye)

Amini amini, tuko pamoja safarini

Wala sigeuki, nipo makini na wenye chuki

Hivi ujabaini? Wanakudanganya maneno lukuki

Eti napenda chini, eti nakuhasi na hugutuki

Hivi inaingia akilini, Ni muda gani na ni lini?

Siku hiyo hatukuwa pamoja? Kama si huzushi ni nini?

Wanga wanajikongoja navyokupenda kwa ukalando

Mwana wametunga hoja, tutengane iwe furaha

Iwe tazamia vioja, usiwaamini mara moja

Wengi ni vizabi zabina, wapiga majungu na wafitina

Magwiji washirikina, pima vyema tena kwa kina

Tusije tukaachana, tutawapa msemo wageni iwe meno

Itakuwa haina maana, mara tu tumefarakana

Pia itakuwa aibu, tujaribu kuvumiliana

Mapenzi ni taratibu, mambo ya jana sio ya leo

Tusije tukaharibu, hebu sikia sogea karibu

Nani wa kunigiribu? Kwako sioni, sisikii

Ukiacha utaniadhibu, we nipe raha, nipe dhabibu

Mpaka ntakapokufa, tushirikiane kuziba ufa

Wanga wasitufate, nafurahi unavyonipenda

Usije ukasema asante, we nipe denda, nipe mate

Mama subiri fungate, mzizi wa fitina tena tukate

Wewe na mimi (Mimi), niko radhi kula yamini

Wewe na mimi (mimi), mama Lily hebu niamini