Ndio Mzee

By Prof. Jay

Thumbnail

Naam ndugu wananchi, MC wenu Babu Ayubu

Ninawaleteeni habari japo kwa kifupi kuhusiana na huyu mgombea wetu bwana Joseph Haule

Mpeni kura za ndiyo kwasababu yeye ni mpenda watu, ni mpenda amani

Na ni mtu mwenye huruma kwa wananchi wote

Kwa hivyo basi nawaomba ndugu wananchi, mumpe kula ili aingie

Naam basi, hivyo basi ndugu wananchi

Eeh, tafadhali namkaribisha mgombea wetu Bwana Joseph Haule

Ili aje aweza kuzungumza na wananchi, karibu

Okay, okay

Naitwa Joseph Haule, mwana wa Msulopo Kianzi

Nadhani nimeletwa niokoe hiki kizazi

Mimi ni mwanasiasa niliyebarikiwa na Mungu

Nimeletwa kwenu muungwana niwapunguzie machungu

Mimi ni mteule kusini mwa jangwa la sahara

Ndiyo maana nimetunukiwa cheti cha juu cha utawala

Na hekima kuliko Mfalme Suleiman, msiwe na wasi

Na hili nitalidhihirisha pindi mtakaponipa nafasi

Actually, nimedhamiria kuwasaidia

Taifa lenye nguvu duniani liwe Tanzania

Jamani, makofi tafadhali basi jamani!

Ni mambo madogo tu

Nadhani nitarekebisha mkinipa visiku vichache tu

Uchumi utapanda ile ghafla bin-vuu

Nataka mpaka Matonya afundishe chuo kikuu

Nchi ya Tanzania itang'ara ile kishenzi

Na nitahakikisha kila bar-maid anamiliki benzi

Si mtafurahi dada zangu jamani? Ndiyo

Basi endeleeni kunisifu kwa nyimbo na mapambio

Nipeni hiyo nafasi jamani, hamwoni hali ni mbaya?

Nataka kuigeuza Tanzania kama Ulaya

Cha kwanza nitakachofanya nitafuta umaskini

Wanafunzi mkafanyie practical mwezini

Kwenye mahospitali nitamwaga dawa kama mchanga

Na nitafungua akaunti kwa kila mtoto mchanga

Mabomba yatatoa maji na maziwa nchi nzima

Watu wa vijijini mtasahau habari za visima

Nitafadhili wachawi waweze kutengeneza ndege

Kila mtu awe na yake makonda na wapiga debe

Si mtafurahi watanzania jamani? Ndiyo mzee

Si ni kweli nakubalika jamani? Ndiyo mzee

Basi mimi mkombozi wenu jama, ndiyo mzee

Na nitafuta shida zenu zote, ndiyo mzee

Hivi ni nanii? Ni vijimambo, ndiyo mzee

Na vinanikera kweli kweli mimi, ndiyo mzee

Basi hali itabadilika sawa? Ndiyo mzee

Na hatamu tutaishika okay? Ndiyo mzee

Wafanyakazi wa serikalini nashangaa hamna magari

Yaani hata mikweche? He-he! Hii ni hatari

Ninampango wa kuongeza mishahara iliyo minono

Mara mia ya ile ya mwanzo iliyofanya mfanye migomo

Nitawapa nyumba nzuri na magari ya kifahari

Watu watashangaa mtakapopita kila mahali

Mkulima kila mmoja nitampatia trekta

Nadhani hiyo kidogo itasaidia kunyanyua sekta

Mtauza nafaka zenu bilioni kwa mabilioni

Watu midomo wazi kama wamekamatwa ugoni

Walimu zawadi zenu oh, nimezificha moyoni

Nadhani mtazimia siku mkizitia machoni

We acha tu! Mtafurahi nyinyi

Ila hapo hapamfai mtu mwingine niwekeni mimi

By the way, polisi wote mi' nawasifu

Jinsi mnavyokwenda sahani moja na wahalifu

Sasa kila mmoja nitampatia helikopta

Nadhani hiyo wote hapo hamjawahi kuota

Raia wa Tanzania mtalala milango wazi

In fact, nina uhakika wa kudhibiti ujambazi

Nitajenga barabara tano-tano juu na chini

Nitajenga kumbi nyingi sana za starehe baharini

Ninaupendo kuliko mshumaa, kumulikia wenzangu

Mtakaoyumba kiuchumi, tutagawana vya kwangu

Si mtafurahi watanzania jamani? Ndiyo mzee

Si ni kweli nakubalika jamani? Ndiyo mzee

Basi mimi mkombozi wenu jama, ndiyo mzee

Na nitafuta shida zenu zote, ndiyo mzee

Hivi ni nanii? Ni vijimambo, ndiyo mzee

Na vinanikera kweli kweli mimi, ndiyo mzee

Basi hali itabadilika sawa? Ndiyo mzee

Na hatamu tutaishika okay? Ndiyo mzee

Ndugu wananchi, kuna mtu ana swali kutoka kwa mgombea?

Nauliza hivi, kuna mtu ana swali?

Basi ajitokeze ili aweze kuuliza swali

Nyie ndugu zangu huyu msimpe uongozi, siyo vizuri

Muongo tu, mnafiki na kiburi kimsuli

Anaongopea sana! Sijui kazaliwa muda gani, alfajiri au alasiri?

Au wakati mvua zile, za kipendi kile?

Amepita pita school lakini mambo yake si mazuri

Wala tusimtetee, atatuangamiza

Labda tusubiri kwanza uchaguzi umwekwisha

Tumemfuma wenyewe kwa Kalumanzila anasafishwa

Kalumanzila akamwambia, "Ehe, shida yako?

Elezea fasta fasta kabla jini hajapanda"

Hajakaa vizuri mashetani si yakamuanza!

Kamsukuma kwa kasi ya kimbunga amejichanja

Tulimsikia akisema kwa sauti kubwa ya kukaripia

"Waungwana! Munisaidie, Ndiyo, nitamweleza!"

Uongo mtupu babake ameibiwa

Waungwana wamempeleka jau mpaka kaibiwa

Yupo-hamna gepu na bugzi! Amewehuka!

Hajatulia huyu mpepeni!

Ni sauti iliyosikika kutoka kwa mzee wa pembeni

Sijui msaidizi, mganga au mpelelezi

Na kwa taarifa yako uongozi hupati ng'o!

Labda urudi kwenu uende ukavunje tunguri

Na hao waganga wako waeleze hupati kitu apa

Hata utoe chapaa

Je wananchi mmenisikia? Ndiyo mzee

Kwa huyu jamaa hatufai, ndiyo mzee

Na inafaa kumchukia, ndiyo mzee

Hatumtaki aondoke zake, ndiyo mzee

Tusimkubali na maneno yake, ndiyo mzee

Tunahakikisha 'atumchagui, ndiyo mzee

Kwasab' jamaa ni mnafiki, ndiyo mzee

Asitufanye tuwe na dhiki, ndiyo mzee