Nang’atuka

By Prof. Jay

Thumbnail

Yeah

Napiga goti natubu

Kwa mungu wangu na jamii

Nimefanya mambo mengi

Kwa kutumia cheo

Naamini cheo dhamana

Nisamehe nisamehe

Nang'atuka nimeshaikosea jamii nikajiita mungu mtu nikajiita nabii

Mwenyeenzi kumbuka na nafsi hii

Napiga goti natubu daima nitakusihi

Nang'atuka nimeshaikosea jamii

Nikajiita mungu mtu nikajiita nabii

Muda sasa umewadia ndugu zangu watanzania

Mambo niliyoyafanya hayapaswi kusimuliwa

Tangu nilipoomba kura kwenye ndio mzee

Mkanipa na kusababsha uchumi ulegee

Kura zikawa kula nikaishi kwa mlungula taratubu nikaanza kubadili mfumo na sura

Nasisitiza sana masuala ya ajira

Kumbe uongo nikaanza kugawa vyeo kwa hila

Hata mashori wangu niliweka mataahira na kusababsha uongozi wangu upoteze dira