Hapo Sawa

By Prof. Jay

On Hapo Sawa

Released on October 13, 2013

Thumbnail

[Chorus]

Kindergaten mpaka chuo kikuu; downtown

Kwa machizi na masister duu; mikono juu

Hapo vipi? hapo sawa!

Hapo vipi? hapo sawa!

Hapo vipi? hapo sawa!

Hapo vipi? hapo sawa!

Magharibi mpaka nyanda za juu; kanda ya ziwa

Kaskazini mpaka East Zoo; I'm coming through

Hapo vipi? hapo sawa!

Hapo vipi? hapo sawa!

Hapo vipi? hapo sawa!

Hapo vipi? hapo sawa!


[Verse 1]

Upper cut chembe kidevu; lazima hukae

Nachana zaidi ya wembe kama mwerevu usinishangae

Mi si kiongozi napigania ukombozi

Nakaba kooni zaidi ya jinamizi kwenye njozi

Nasaka haki sio kilio cha samaki;

Machozi kwenda na maji

Hiki kipaji sio bahati

Akili yangu sio uwanja wa majaribio

Neno langu linaongeza faraja kwenye vilio

Nafikiri nifike, sisemi tu nisikike

Jasho langu linafanya malengo niyafanikishe

Niko tayari kwa heri ama kwa shari

Jino kwa jino ukimwaga mboga namwaga ugali

Maisha yenyewe kamari hatari ndani ya safari

Kichwani vina kama mchanga wa bahari

Huyu ni Mwibili wangapi mnawabashiri

Na kuwavisha mataji kwa vina vya tafsiri


[Chorus]

Kindergaten mpaka chuo kikuu; downtown

Kwa machizi na masister duu; mikono juu

Hapo vipi? hapo sawa!

Hapo vipi? hapo sawa!

Hapo vipi? hapo sawa!

Hapo vipi? hapo sawa!

Magharibi mpaka nyanda za juu; kanda ya ziwa

Kaskazini mpaka East Zoo; I'm coming through

Hapo vipi? hapo sawa!

Hapo vipi? hapo sawa!

Hapo vipi? hapo sawa!

Hapo vipi? hapo sawa!


[Verse 2]

Ili nifanikiwe nahitaji marafiki

Ili nifanikiwe zaidi nahitaji maadui

Mkononi sina tattoo bali nina alama ya ndui

Mtanzania namba moja majungu hayasumbui

Mchaka mchaka nakimbiza kila upande

Simtumikii kafiri ili charti yangu ipande

Get off my shoulder ngoma inavuka border

Muda unazungumza wa mia hapati moja

Pori kwa pori hapa beep mmebaki story

Kama zama za mtikila na sera ya kabacholi

Naishi biashara daima siogopi hasara

Na mara kwa mara hii busara huepusha madhara

Napoza nile kama nahisi cha moto

Napokea matatizo yangu kama changamoto

Nipo ili nife nanena bila kificho

Naitunza heshima yangu zaidi ya mboni ya jicho


[Chorus]

Kindergaten mpaka chuo kikuu; downtown

Kwa machizi na masister duu; mikono juu

Hapo vipi? hapo sawa!

Hapo vipi? hapo sawa!

Hapo vipi? hapo sawa!

Hapo vipi? hapo sawa!

Magharibi mpaka nyanda za juu; kanda ya ziwa

Kaskazini mpaka East Zoo; I'm coming through

Hapo vipi? hapo sawa!

Hapo vipi? hapo sawa!

Hapo vipi? hapo sawa!

Hapo vipi? hapo sawa!


[Verse 3]

Wewe bora mwanamziki; mimi mwanamziki bora

Chance zetu hazifanani kama mafua na ebola

Mwenye hekima huona haja na kijificha

Bali mpumbavu huenda mbele na kuvimba kichwa

Nani anabisha? simama kudhibitisha

Niite mwanaharakati hip hop naiwakilisha

Fanya ufanyavyo akili yangu haiko petty

Unataka kuwa Jay copy kama double decki

Siui mende kwa nyundo maana nitaumia mimi

Na ndiyo maana nawadharau mnaotaka beef na mimi

Born town kitambo utanieleza nini?

Wakati huo wengine wenu hata hamjakuja mjini


[Chorus]

Kindergaten mpaka chuo kikuu; downtown

Kwa machizi na masister duu; mikono juu

Hapo vipi? hapo sawa!

Hapo vipi? hapo sawa!

Hapo vipi? hapo sawa!

Hapo vipi? hapo sawa!

Magharibi mpaka nyanda za juu; kanda ya ziwa

Kaskazini mpaka East Zoo; I'm coming through

Hapo vipi? hapo sawa!

Hapo vipi? hapo sawa!

Hapo vipi? hapo sawa!

Hapo vipi? hapo sawa!

Kindergaten mpaka chuo kikuu; downtown

Kwa machizi na masister duu; mikono juu

Hapo vipi? hapo sawa!

Hapo vipi? hapo sawa!

Hapo vipi? hapo sawa!

Hapo vipi? hapo sawa!

Magharibi mpaka nyanda za juu; kanda ya ziwa

Kaskazini mpaka East Zoo; I'm coming through

Hapo vipi? hapo sawa!

Hapo vipi? hapo sawa!

Hapo vipi? hapo sawa!

Hapo vipi? hapo sawa!