Last Interview

By Munta Dee

On Me Sio Tozzy

Released on March 15, 2026

Thumbnail

#Intro

Badi ubadani Soundbox 7

Dreams Records

Wish your boy viddy viddo boy baba ake na JJ

Ebwana leo tumemweka mtu kati

Munta Dee

Yanayosemekana mtandaoni na mtaani

Yakuwa kwamba yeye anawavimbia wasanii

Hivi ni kweli?

#verse

Najipa maua yangu mwenyewe jipeni kiki

Muziki umechange madogo jipeni bichi

Muda unaongea mtajua mbivu na mbichi

Na nani ambaye anawasumbua kipindi hichi

Wananiundia tume bado hawajitume

Yaani wanakunja utasema sio wanaume

Na kama wana blessing nikipata vipi wanune

Mi kunishusha labda waje kinyume nyume

Nawakimbiza michano na singeli laza

Si copy cha mtu mimi sio msanii wa cover

Mambo ya mabifu hata dini imekataza

Mkipanga list mimi ndio wa mwisho na wa kwanza

Sawa sawa Munta Dee

Umesema mambo mengi mengi sana

Lakini Watanzania wamekupa sikio kuweza kukusikiliza

Muziki mzuri unaofanya

Je mategemeo yako ni nini?

#verse

Kama mkitoa tuzo zifuatazo nipe mimi

Tuzo ya kutoa hit msafara nipe mimi

Tuzo ya kurusha bendera mbagala nipe mimi

Na tuzo msanii bora wa mwaka nipe mimi

Nataka kuiweka singeli kwenye tuzo za BET

Maana siimbi makelele kama vile naniliii

Yaani kama hamtojali basi tufanye hivi

Mimi nikikaa pembeni na wa kuchangamsha game nani

Na ahidi nitauweka muziki mahali pema

I mbili sita nimeanza tu mitano tena

Mimi ndio nafanya waliotoka washindwe kuhema

Na kama una swali jingine niulize tena

Sawa nimeridhishwa na majibu yako

Lakini ukweli haya mambo yote yanaendelea

Kiini chake unayajua we mwenyewe

Sasa una lipi la kuwaambia mashabiki zako na wanaokusikiliza?

Naanza kutuma salamu kwa wote walionikataa

Mitaa inapata utamu toka kwa mtoto wa kitaa

Mungu ndio mtaalamu kwani nani anakataa

Nachoshwa na hizi fununu wasilete u superstar

Kwanza ulinzi uimarishwe na polisi

Naona watu wamepandwa na ibilisi

Ilipotoka mpaka hapa haikuwa rahisi

Maisha tume risk na bado tunaishi

Kuanguka sio kuteleza swali ni meza

Sidi anakunja wakati anapendeza

Macho unafumba au unataka kunikonyeza

Ngoma unacheza japo kuwa ngumu kumeza

#Outro

Matozy sio mimi yeye tu wa

Kama napita Man

Badi ubadani Soundbox 7