Tuachane

By Lava Lava

Released on May 22, 2017

15K Views

Thumbnail

[Intro]

Aaaaah Aaaah Aaaaah Aaaah


[Verse 1]

Kama imeshindikana kunirudia, isiwe taabu

Usiuforce moyo kupenda usipostahili

Ya nini kung’ang’ania, nishachoka kuwekwa sub

Siwezi ooh, na mapenzi nishaghaili

Tena niko tayari vipigwe vinumbi, kengere kwa sherehe

Kinaghaubagha mbele ya umati tuachane

Na kama hautojali, tuite waumini, mapadre na masheikh

Yaishe, labda sa kwa nini tutesane

Kweli we ndo nikupendae, ila unanipa ghadabu jina

Tusitoane nyongo

Na kama umenichoka, eh niache kistarabu jina

Usinipe chongo mie


[Bridge]

Mwili umebaki kongoro, nyama sina ni mifupa

Naiona ndomboro kabisa, siwezi furukuta

Penzi kiporo, limeshachina linanuka

Huishi kokoro, purukushani kutwa kucha iyeeh


[Chorus]

Bora tuachane, bora tuachane, siwezi

Bora tuachane, yamenishinda mapenzi

Mi naona bora tuachane, eeh tuachane, siwezi

Bora tuachane, yamenishinda mapenzi


[Verse 2]

Ni dhahiri kisima kimekauka maji

Ndo maana naona kata, sina maana tena

Nilifikiri mi gonjwa langu limepata mponyaji

Umeniongezea homa, mwili wote wantetema

Mi naona basi labda si ridhiki yangu

Kama hunitaki, acha tu niende zangu

Ya nini mishikaki, ntatafuta boda yangu

Nijinafasi niipande peke yangu


[Bridge]

Mwili umebaki kongoro, nyama sina ni mifupa

Naiona ndomboro kabisa, siwezi furukuta

Penzi kiporo, limeshachina linanuka

Huishi kokoro, purukushani kutwa kucha iyeeh


[Chorus]

Bora tuachane, bora tuachane, siwezi

Bora tuachane, yamenishinda mapenzi

Mi naona bora tuachane, eeh tuachane, siwezi

Bora tuachane, yamenishinda mapenzi