Njiani

By Ksonrap

Thumbnail

Njiani sio pouwa njiani kunavituko

Njiani kuna milupo njiani kuna machoko

Njiani kuna watoto wenye kiburi

Hawajui mwisho wayote nikaburi

Njiani nimekutana na mabaya na mazuri

Nimepita njia za hatari mchana jua kali

Bila ya mti wenye kivuli njia chororo kali

Nikakutana nakabali yani roba ya mbao mixer misumari..

Nimekutana na mateja alosto kali

Kuna mapusha vijana hawana kazi wanacheza tu kamari hatari..

Niona makatili wanapora majerui

Ajali..nimeona manabii wauongo wanahubiri wazipate tu salari.. police nao wanazifinya sana hongo dili za michongo dawa za asili mkongo..

Kuwengeni wanamsongo wamawazo..

Wengine wamelogwa wanaokota tu makopo...

Hali inatisha vibinti vinadanga..

Giza limetanda chozi linatoka wengine wamezaa nakutupa tu vichanga..

Kijijini hakuna umeme wala maji mbunge wenu yupo huku town anatamba..njiani kunavisa na visanga machinga hana mtaji bado anajichanga..akizipata mgambo kwenye jiji vitu vyake anavimwaga..