Hey jay!

By J93

Released on November 10, 2017

Thumbnail

INTRO(J93)

Let me talk to my soul(let me talk to ma soul)

Let me talk to your soul(let me talk to your soul)

Let"s talk to our souls(let's talk to our souls)

VERSE 1(J93)

Hey jay, kumbuka ulikuja peke yako jay

Na utaondoka peke yako jay

Maisha hayana promo so usipende kujishusha jay

Fanya unachoweza usikufuru jay

Ongea na MUNGU wako ndio boss jay

Akupe neema ili uweze pata jay

Usiogope loss ukitaka fanikiwa jay

Usichachawe wakikutenga jay

Wala usichukie wakikuponda jay

Kamwe huwezi ona chogo lako jay

Kama wana diss hadi MUNGU wewe ni nani jay?(wewe ni nani wewe ni naniii)

Penda nafsi yako

Penda MUNGU wako

Hata na jirani yako jay

Kufanikiwa ni hatua jay

So pambana usipende shortcut jay

Usibabaike na uzuri jay

Wengi wao mashetani jay(mashetani mashetani)

Njia yao ni ya moto jay

Usifatane nao wanaotangaza wameokoka jay

Maana wamevaa vya ukoka

Hawaogopi mpaka MUNGU wanamkopa

Nusu binadamu nusu nyoka

Usistuke pale wote wanapokugeuka

Jay wapo watao kuchukia

Bila sababu hata na tatizo pia

Wengine michongo watakanyagia

Ili wewe ukose so furaha kwao hutimia(hutimiaa)

Kuna kichwa na mkia

So mtoto anaweza lisha familia

Utaishi mara moja changamka nini unangoja jay?