Dollar Moja

By J93

Released on February 11, 2023

Thumbnail

Verse 1 (J93)

Yeah

Pindi wewe umekesha bar

Na wanangu tumelala njaa

Nguo zetu ndio zimechakaa

Kuu Kuu hazifai hata kuvaa

Mishe ndio adimu yani hakuna

Ukipata leo kesho Huna

Jiko linazidi tu kununa

Inabidi uforce upate kutafuna

Tunakula raka moja tu

Ugali nyanya chumvi kitunguu

Tupo kama watu kumi duu

Ili tu ushibe weka maji Juu

Nooo

Tumejichokea

Ni magumu yanatuelemea

Kote Giza wapi tutaelekea

Dollar moja ndio tunapotokea

Chorus ( Melloh)

Dollar moja

Dollar moja

Dollar moja

Dollar moja

Verse 2 (J93)

Wewe ndio baba kiongozi home una Familia

Kwenu ndio wa Kwanza una Madogo wote wanakuangalia

Akili zao baba ametoka kwenda kututafutia

Nikirudi shule kama kawa ugali unanisubiria

Unaenda mishe hupati hata Mia

Umbali mrefu sana umetеmbea

Unakaa chini unaanza tu kulia

Ya dunia yamekuelеmea

Maisha kwetu bado ni magumu

Njaa daily inatuhukumu

Mpaka unatamani kunywa sumu

Getto kwa machizi Huwezi afford room

Chorus (Melloh)

Dollar moja

Dollar moja

Dollar moja

Dollar moja