Watoto wangu nyie mimi baba yenu

Nina nguvu sana za kuua hata simba

Simba na makali yote

Akimuona tembo anachimba

Ila hainivimbishi kichwa

Nachapa kazi siendekezi majungu

Ridhiki anayegawa ni Mungu

Eti niende kwa mganga piga nyungu

Nimroge fulani awe pungua

Mungu akikupa kilema lazima atakupa na mwendo

Lipiza mabaya kwa wema kula maisha bila upendo

Kumdharau usiyemjua ni dhambi, dhambi

Mtangulize Mungu na dua popote kambi, kambi

Yeah this life is a gamble

Basi jitahidi kuwa humble

Usimdharau mama wa kambo

Huenda alisha kusifu kitambo

Ni usia (Huu ni usia, usia wa tembo)

Hii dunia tunapita (Huu ni usia, usia wa tembo)

Usiendekeze vita (Huu ni usia, usia wa tembo)

Usijione special special (Huu ni usia, usia wa tembo)

Ju hauijui kesho kesho kesho

Ukikosa elimu bora sio mwisho wa maisha yako

Na kuishi chini ya dola

Wala hailkuwa matakwa yako

Cha mtu ni mavi

Achana nacho tafuta chako hata kichelewe

Uwе na meza ama jamvi ridhika na ulichonacho

Omba kwa Mungu upewe

Kingi, usijionе queen ama kingi

Nakujisifu akili nyingi

Kisa unamiliki shilingi, shilingi

Mmmh punguza idadi ya maadui

Maana atakaye kuzika humjui

Mwambieni huyo kaka anajiita chui

Aache kudandia bifu chanzo hukijui

Kumdharau usiyemjua ni dhambi, dhambi

Mtangulize Mungu na dua popote kambi, kambi

Yeah this life is a gamble

Basi jitahidi kuwa humble

Usimdharau mama wa kambo

Huenda alisha kusifu kitambo

Ni usia (Huu ni usia, usia wa tembo)

Hii dunia tunapita (Huu ni usia, usia wa tembo)

Usiendekeze vita (Huu ni usia, usia wa tembo)

Hakuna haja kuduniashiana misuli (Huu ni usia, usia wa tembo)

Dunia hakuna anayeijua vizuri

Zaidi ya Mungu baba, Mungu baba baba

Usia wa Tembo, Konde boy