[Intro]

Big boy

(Instrumentals)

Mmm

Mmm


[Verse 1]

Ana ka sura ka upole

Miaka nenda rudi hazeeki

Tena ni mtu wa gym, gym

Shepu ndio linanipa wazimu, zimu

Na tattoo nimchore

Ila' ndio hivyo tena, hapendeki

Ama kweli mapenzi hayana mwalimu

Wengine hata kuniona ni adimu

Hivi tuseme ana ngekewa

Ama nyota yake kali ananizidi

Ama mjini nimechelewa

Mbona wengine wanamponda wanamuita bibi

Nilianza kumuona mapema

Enzi za mabanda ya sinema

Alikuaga ni rafiki na Wema

She's so cute


[Hook]

Acha wanione mshamba tu

Tuta huwezi kulipigia honi

Umri nao ni number tu

Kinachoniuma anajifanya haoni


[Chorus]

Kama unamjua (Mtaje)

Nani anaye mjua? (Mtaje)

Kama unamjua (Mtaje)

Avimbe kichwa, ajisifie

Basi, kama unamjua (Mtaje)

Kama unamjua (Mtaje)

Kama unamjua (Mtaje)

Avimbe kichwa, ajisifie

Mm-mmmh


[Verse 2]

Anaye lenga kwa ruler

Siku zote ndo apataye

Mwambieni mwanangu Paula

Mi nampenda mamae

Tena ni fundi wa kuchanua, Aah

Utasema samaki ng'onda

Hapo ndio nikagundua, Ah

Nini kiliwaliza makonda

Wa dala, dala, dala

Mi nashindwa kulala, lala, lala

Hana mbadala, dala, dala

Anaitwa Ka-, Ka-, eh

Hakika ye ndio kiboko yangu

Jua likiwaka, ikinyesha

Utembo na ujeshi wangu

Getini kwake nilikesha

Mtihani wa mapenzi hakuna aliye fuzu

Sawa na unywe pombe na useme una udhu

Na mtu ukishapenda unakuwa zuzu

Eti nawaza aje kuwa mama Zuzu


[Post-Chorus]

Kama unamjua (Mtaje)

Kama unamjua (Mtaje)

Kama unamju-, (Mtaje)

Avimbe kichwa, ajisifie


[Outro]

Eh, Big boy na Migo wanamjua

Cha upole anamjua

Uncle Duke naye anamjua

[Saraboy] na Chengo wanamjua

Hadi Sekela wa mipango anamjua

Big Poppa, Mtambele wanamjua, ah

Eh, eeh-eeh